Unknown Unknown Author
Title:
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
HOME COMMONWEALTH NA UKOLONI MAMBOLEO Hivi karibuni katika baadhi ya nchi za Afrika kumekuwa na mijadala baina ya viongozi wa siasa,...
HOME

COMMONWEALTH NA UKOLONI MAMBOLEO

Hivi karibuni katika baadhi ya nchi za Afrika kumekuwa na mijadala baina ya viongozi wa siasa, mabunge nk. kuhusu kuhalalisha ushoga (homosexuality) na hata uchangudoa (prostitution).

Aliyewahi kuwa rais wa Botswana alitoa wito kwa serikali ya Botswana kuhalalisha ushoga na uchangudoa (pitia USHOGA NA UCHANGUDOA BOTSWANA hapo chini). Nchini Zimbabwe kulikuwa na malumbano kati ya vyama vikuu viwili vya siasa kuhusu haki za mashoga. Nako nchini Uganda kulianzishwa mjadala bungeni kuhusu swala hili.

Cha kushangaza mijadala hii ilikuwa ikiendeshwa kwa kasi ya ajabu, wengine tukishangaa nini chanzo cha mijadala hiyo! Kwani siku mashoga wapo mfano Tanzania,Kenya nk. na hakuna anaye bugudhiwa kwa kujihusisha na mahusiano hayo.

Lakini siri ya mijadala hiyo imefichuka, kumbe viongozi wa nchi wanachama wa Commonwealth waliweka majukumu ya kutimiza, mojawapo ni kuhakikisha haki za binaadamu katika nchi zao linatekelezwa. Jukumu hili linagusa mambo mengi likiwemo haki za mashoga, ndio maana mijadala imekuwa mingi! Kwanini viongozi wetu awakusema chanzo ni nini?

Hivyo basi sababu swala la ushoga alijapewa uhuru unaostahili, viongozi wa nchi hizo ikiwemo Tanzania wamepigwa mkwara na Waziri mkuu wa Uingereza (nchi inayotoa misaada kwa nchi wanachama wa Commonwealth) kwamba wasipotekeleza majukumu yao haswa la kuwepo kwa haki za mashoga, misaada itapunguzwa kama sio kufutwa (http://www.bbc.co.uk/news/uk-15503837 ) !

Kumbe nchi zetu zimepata uhuru wa bendera tu, sababu baadhi mipango ya kuendesha nchi inatoka kwa nchi iliyokuwa  mkoloni? Kwanini viongozi wetu hawaotoi mikakati ya namna ya kutatua matatizo ya nchi zao kwenye vikao vya umoja huo na kukataa kuburuzwa? Badala yake wakirudi nchini wanajitapa kwenye majukwaa.

Ni aibu kubwa! Tanzania inasherehekea Miaka 50 ya kujitawala ama miaka 50 ya kupokea misaada na kupangiwa majukumu?  Viongozi wetu wanaendekeza ukoloni mamboleo!

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top