HOME
Uchumi wa Tanzania unaodhaniwa kukua ni ukuaji wa takwimu ilhali hali halisi ya maisha ya watu inasikitisha. Ukiangalia bajeti za taifa miaka yote tangu uhuru, muungano na hata sasa, utagundua kwamba kuna nakisi ya bajeti inayotegemea misaada, mikopo na hisani ya wahisani na wale wanaoitwa wabia wa maendeleo. Ukweli ni kwamba, Tanzania inaongozwa na viongozi wachovu wa kuongoza!
Uchovu wa akili ya uongozi unajengwa na dhana kwamba ‘watu ni walewale wenye uwezo uleule na wanaongoza vilevile kama walivyozoea.’ Kama dhana ya umasikini Tanzania (Tanganyika), ilitangazwa tangu tulipopata uhuru mwaka 1961 hadi sasa!
Umasikini umekuwa wimbo wa taifa. Ukiachilia harakati zote za chama kuanzia TANU, ASP hadi CCM wanaoongoza serikali kwa sasa, Tanzania bado ni masikini. Viongozi ni walewale, na fikra zao ni zilezile za kutegemea misaada na mikopo ya wahisani na wakopeshaji (wanyonyaji) kinyume na dhana ya uhuru kamili.
Uongozi wa Tanzania, kwa sasa, unaendeshwa na viongozi wasiozingatia dhana ya uongozi. Viongozi wameshindwa kuonyesha njia. Hakuna viongozi wenye utayari na hiyari ya kuwaelekeza wananchi katika kufikia utashi wa kupambana na umasikini wa kipato cha mtu binafsi, kipato cha kaya, kipato cha jamii, na hatimaye kipato cha taifa.
Viongozi wengi wamekuwa wategemezi wa fikra za kukopa na kuwapa kipaumbele wawekezaji wanyonyaji kwa gharama ya rasilimali za taifa.
Tanzania ilipofika imeachwa kama shamba la bibi au kituo cha majaribio ya uongozi ulioshindwa kusimamia rasilimali za nchi; yaani, watu na ardhi. Viongozi walioshindwa kutokana na uchovu wa akili wamekuwa wakitumia akili ndogo iliyochoka na isiyokuwa na manufaa kutokana na aidha uchukuzi wa upumbavu au upumbavu kamili (kwa mujibu wa kanuni ya Mendel) kuongoza nchi kwa mazoea hata kama viongozi hao hawana tija kwa watu na nchi kadhalika.
Tazama, pamoja na utajiri wa rasilimali ardhi na watu, Tanzania imeshindwa kuhakikisha usalama wa chakula kwa watu wake. Kushindwa kwa uongozi wa nchi kuhakikisha usalama wa chakula kwa wananchi, kwa sehemu kubwa ni matokeo ya kushindwa kwa akili ya uongozi katika kutunga sera madhubuti za kilimo, chakula na lishe; kusimamia utekelezaji wa sera hiyo; na kuhakiki kiasi na ubora na usalama wa chakula kwa wananchi wa Tanzania.
Tazama, ukisoma taarifa ya demografia ya hali ya afya Tanzania ya mwaka 2010, inaonyesha kwamba, asimilia 42 ya watoto chini ya miaka mitano wamedumaa kutokana na ukosefu wa chakula na lishe bora (TDHS, 2010).
Hii ina maana kwamba, katika kila watoto 100, watoto 42 wamedumaa. Madhara ya kudumaa kwa watoto hawa ndiyo ongezeko la wananchi watakaokuwa wachovu na au walemavu wa akili baada ya miaka 15 ijayo!
Kuporomoka kwa kiwango cha elimu na ufaulu kwenye elimu ya msingi, sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu kwa sehemu kubwa ni matokeo ya umasikini wa kipato unaochagiza wananchi wengi kukosa chakula na lishe bora inayowalazimisha kula ili kushiba na si kula kwa afya ya mwili na akili.
Haya ndiyo matokeo ya sera mbovu za kilimo, chakula na lishe isiyozingatia uhalisia wa mahitaji halisi ya wananchi kwa rika zote; yaani, watoto, wanawake na vijana.
Kwa mwendo huu wa uongozi kushindwa kusimamia uchumi kwa maendeleo ya watu na miundombinu ya kiuchumi na kijamii, Tanzania inaangamia kwenye umasikini wa kutegemea akili za kushikiwa na au akili za kuazima kutoka kwa wahisani.
Wahisani ndio wanaoongoza nchi kwa kuwa imewekwa rahani kwa mikopo na misaada ya wakopeshaji na wahisani! Huu ni uchovu wa akili unaoatamizwa na akili ya uongozi wenye mawazo ya utumwa mamboleo kwa akili za kushikiwa. Uhuru wetu umeporwa kwa nchi kuwa mdaiwa na kwa utegemezi wa bajeti ya kukusanya ndiyo matumizi ilhali asilimia zaidi ya 30 ikiwa misaada kutoka nje.
Tujisahihishe (1962), Azimio la Arusha (1967), Mwongozo wa TANU (1971), Uhuru ni Kazi (1974), Elimu ni Kazi (1974), Hotuba ya Rais katika Bunge (1975), Mwongozo wa CCM (1981) na makabrasha mbalimbali ya sera na mipango ya utekelezaji tangu 1961 hadi sasa, yalidhamiria kuatamiza fikra za kujitegemea.
Hata hivyo, viongozi wetu wameshikwa na ugonjwa wa ‘upumbavu uliopitiliza’ kwa kukubali akili zao zitawaliwe na fikra za utegemezi wa akili za kushikiwa na kudhani kwamba misaada, mikopo na uwekezaji wa kigeni ndio utakaomaliza umasikini wa Tanzania! Haya ni mawazo ya kijinga na upumbavu uliopitiliza (rejea Nyerere, 1962 na 1992).
Tanzania imekwama na imekwamishwa na uongozi unaotumia akili ndogo na watu wanaodhani kwamba maendeleo yataletwa na fedha za mikopo na uwekezaji. Huku ni kufilisika; na wale wenye fikra za aina hii ni muflisi.
Kamwe, na kwa muktadha wa maendeleo endelevu ya Tanzania, hatuwezi kutoka hapa tulipokwama hata pale tutakapojikwamua na fikra mgando. Viongozi wenye akili ndogo na wenye uchovu wa akili ni wajibu wawajibishwe kwa kushindwa kwao kutimiza ahadi walizochukua katika kuwatumikia wananchi. Ni wajibu usioepukika kwa kila mwananchi kukubali mabadiliko.
Mabadiliko ya haraka yanahitajika ili kuondoa mfumo wa uongozi unaotokana na muundo ulioatamizwa na uchovu wa fikra kwenye kuongoza uchumi, jamii na siasa. Kama nchi itaachwa iongozwe na viongozi walioshindwa kwa jinsi ileile ya kushindwa kusimamia rasilimali za nchi, kuna hatari Tanzania ikashuhudia kuporomoka kwa haiba yake kisiasa na hatimaye kuparaganyika kwa mujtamaa wa kijamii.
Ongezeko la deni la taifa ni ushahidi wa dhahiri, na hali ya kudumaa kwa uchumi kutakwenda sanjari na kudumaa kwa akili ya viongozi wa sasa na baadaye kadhalika.
Ni wajibu kwa kila mwananchi mahali alipo kusimama kidete kukemea tabia inayoatamizwa na viongozi na watendaji wa serikali kuacha tabia na haiba ya kutumia akili ndogo, ulemavu wa fikra na uchovu wa akili katika kudadavua na au kutatua matatizo ya uchumi wa Tanzania.
Viongozi waonyeshe dhamira ya dhati na madhubuti katika ujenzi wa nchi inayojitegemea kwa matumizi endelevu ya rasilimali za nchi kwa manufaa ya wananchi. Hakuna maendeleo endelevu kama viongozi watashindwa kusimamia rasilimali watu na ardhi katika kufikia mujtamaa wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
UMASIKINI WA TANZANIA: Uchovu wa akili ya uongozi
KWA miaka 50 sasa, Tanzania imeshuhudia kushindwa kwa uongozi kufikia utashi wa uhuru katika kuleta mujtamaa wa kichumi, kijamii na kisiasa. Mwalimu Julius K. Nyerere alifundisha kwamba, ili nchi yetu iendelee tunahitji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora. Tanzania imekwama kwenye umasikini wa kipato cha watu na pato la nchi kadhalika.Uchumi wa Tanzania unaodhaniwa kukua ni ukuaji wa takwimu ilhali hali halisi ya maisha ya watu inasikitisha. Ukiangalia bajeti za taifa miaka yote tangu uhuru, muungano na hata sasa, utagundua kwamba kuna nakisi ya bajeti inayotegemea misaada, mikopo na hisani ya wahisani na wale wanaoitwa wabia wa maendeleo. Ukweli ni kwamba, Tanzania inaongozwa na viongozi wachovu wa kuongoza!

Chapisha Maoni