HOME
Hot News- CHADEMA SHINYANGA WATANGAZA KUFANYA MAANDAMANO KESHO JUMATATU
Habari
zilizokifikia chumba cha habari cha Malunde1 blog ni kwamba kesho
Jumatatu Septemba 22,2014 Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema mkoa
wa Shinyanga kitafanya Maandamano ya amani kupinga Bunge maaalum la
katiba linaloendelea mjini Dodoma.
Maandamanao
hayo yataongozwa na viongozi wa kanda wa chadema,viongozi wa mkoa na
wilaya mbalimbali za mkoa wa Shinyanga yanatarajiwa kuanza saa mbili
asubuhi
Kwa
mujibu wa katibu wa Chadema mkoa wa Shinyanga Zacharia Thomas Obadi
maandamano hayo yataanzia katika ofisi ya Chadema mkoa na kuelekea
katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga ambako watafanya mkutano wa
hadhara.
Katika
taarifa yake ameliomba jeshi la polisi kutoingilia kati maandamano hayo
kwani ni maandamano ya amani yanayolenga kupinga matumizi mabaya ya
pesa za wananchi yanayofanywa na bunge maalum la katiba.
Hata
hivyo akizungumza na Malunde1 blog hivi punde kwa njia ya simu kaimu
kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Mussa Athumani amesema jeshi la
polisi mkoa wa Shinyanga halijatoa kibali kwa chama hicho kufanya kwa
maandamano hivyo kuwataka wananchi kufuata utii wa sheria bila shuruti.
Aidha
amesema jeshi la polisi harijaridhia kufanyika kwa maandamano kutokana
na hali iliyopo nchini na hayo ni maagizo ya jeshi la polisi nchini
kwamba hivi sasa hawaruhusu maandamano kwa ajili ya kulinda amani ya
nchi.
Chapisha Maoni