Jambazi alivamia Benki, walichomfanyia wapita njia ni kali ya mwaka…
Wizi katika benki ni moja ya uhalifu
ambao umekuwa ukijitokeza sana siku hizi hapa Tanzania, ambapo wapo
majambazi wengine baada ya kupora pia wamekuwa wakifanya mauaji.
Hii ni kali.. Kuna video yenye taarifa
kutoka China, jambazi alivamia Benki kwa lengo la kuiba, mmoja ya
wafanyakazi aliposhtukia alikusanya pesa zote na kuzifungia katika safety box, akapiga simu Polisi halafu akajikusanya na wenzake wakajifungia chooni.
Jambazi huyo alipasua kioo na kuingia counter, akaanza kukagua droo kama zilikuwa nna chochote.
Mfanyakazi wa Benki hiyo, Li Dehua amesema
wakati wao wakiwa wamejificha, wapita njia walijikusanya kwa wingi
katika counter za Benki na kumzuia ndani ya Benki hiyo mpaka Polisi
walipofika na kumkamata jambazi huyo.
Chapisha Maoni