HOME
MTANZANIA
Mkusanyiko wa zile Stori zilizopewa Headlines kwenye Magazeti ya leo January 6, 2015 Nimekuwekea hapa
Mkazi wa Kata ya Buhare Manispaa ya Musoma, Helena Paulo mwenye umri wa miaka 21 amejifungua watoto pacha wa kike walioungana kifua na tumbo katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mara.
Kutokana na taarifa za watoto hao
kusambaa mitaani,wananchi walimiminika hospitalini hapo kushuhudia
watoto hao waliozaliwa Januari 4 mwaka huu likiwa ni tukio la pili baada
ya lile la kwanza kutokea Agosti 6 mwaka jana.
Akielezea hali ya pacha mkunga wa zamu
wa hospitali hiyo Elisifa Makala alisema walimpokea mjamzito Helena
January 3 akiwa mwenye uchungu wa kawaida na kuamua kumpumzisha kusubiri
kujifungua kutokana na kutokua na tatizo lolote.
Alisema ilipofika saa 8 usiku alianza
kusikia uchungu ambapo alipewa msaada wa kujifungua lakini alishindwa
kujifungua kwa njia ya kawaida kutokana na mtoto kutanguliza miguu na
kufanyiwa upasuaji ambapo waliwakuta watoto wakiwa wameshikana.
MTANZANIA
Watu 22 wamepandishwa kizimbani katika
mahakama ya jiji la Dar es salaam kwa makosa mawili tofauti,likiwemo la
kufanya biashara ya kuuza miili yao.
Akisoma shtaka hilo mwedesha mashtaka
Ramadhan Kalinga alisema watuhumiwa hao walikamatwa maeneo ya Ubungo na
kwamba walikua wakiuza miili yao huku wakijua kufanya hivyo ni kosa
kisheria.
Washtakiwa walikana na kurudishwa kutimiza masharti ya dhamana na shauri lao litaendelea tena Januari 13 mwaka huu.
NIPASHE
Zaidi ya wafanyakazi 150 wa Shirika la Usafirishaji Dar es salaam ‘UDA’ wamefukuzwa kazi Desemba mwaka jana.
Msemaji wa Shirika hilo George Maziku
alisema wafanyakazi hao wamepunguzwa ikiwa ni moja ya mikakati ya
kuimarisha utendaji wa shirika hilo.
Alisema hatua hiyo imechukuliwa baada ya Shirika kugundua kwamba limeajiri wafanyakazi wengi ambao hawana kazi za kufanya.
“Ni kweli Shirika limeamua kupunguza
wafanyakazi tangu Disemba30 mwaka jana,lengo ni kuimarisha utendaji kazi
na kuongeza ufanisi wa kazi”alisema Maziku.
NIPASHE
Wizara ya fedha imesema hatua za awali
zilizoanza kuchukuliwa na Rais Jakaya Kikwete kushughulikia maazimio ya
Bunge kuhusu sakata la uchotwaji wa fedha zaidi ya bilioni 300 za
akaunti ya Tegeta Escrow zimewezesha wahisani kuanza kutoa misaada
waliyokua wameisitisha awali.
Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mwigulu Nchemba alisema
katika nusu ya mwaka wa kalenda wa fedha kulikua na changamoto nyingi
ikiwemo wahisani kusitisha misaada yao kwa Tanzania kusubiri maamuzi
yaliyotolewa na Bunge kuhusiana na sakata la Tegeta Escrow.
“Kama Taifa tuanze misingi ya
kujitegemea,tumepata fundisho kupanga miradi ya maendeleo halafu
unategemea fedha za wahisani ni tatizo,”alisema Nchemba.
Alisema kutegemea wahisani ni tatizo
ambalo nchi inabidi kujipanga kuondokana nalo kwani hali hiyo
inakwamisha miradi kuchelewa kutekelezwa wahisani wanaposhidwa kuleta
fedha kwa wakati.
NIPASHE
Makabidhiano ya miradi ya ujenzi wa
miundombinu ya gesi asilia,likiwemo bomba la kusafirishia gesi kutoka
Mtwara hadi Dar es salaam kati ya Mkandarasi wa Shirika la Petrol
Tanzania TPDC yanatarajia kufanyika Juni mwaka huu,baada ya kukamilika kwa asilimia 100.
Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC, Michael
Mwanda na Kaimu Meneja mkuu Mhandisi Kapuulya Musomba,mradi huo
ulianzishwa mwaka 2010 mpaka sasa umefikia asilimia 94.
Musomba alisema mradi huo umegharimu dola za Marekani 1.225 ambazo ni zaidi ya trilioni 1.8 ambazo ni za mkopo.
Alisema benki ya Exim ya China imechangia asilimia 95 huku Serikali ya Tanzania ikichangia asilimia tano kati ya fedha hizo.
NIPASHE
Mahakama kuu ya Tanzania imeiandikia
barua Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na uvuvi kwa ajili ya kurejesha mali
ikiwemo meli ya Tawariq na zaidi ya Bilioni mbili za tani 296.3 za
samaki kwa raia wawili wa China.
Kwa mujibu wa barua hiyo iliyosajiliwa
na msajili wa mahakama Disemba 17 imeitaka Serikali kurejea
ahadi,kupitia hati ya kiapo iliyotolewa na Godfrey Nanyaro,Dk Charles
Nyanlundana na Katibu mkuu a Wizara hiyo.
Kwa mujibu wa msajili huyo kiapo
kinasema endapo washtakiwa hawatakutwa na hatia mahakamani Serikali
italipa gharama za samaki waliokutwa nao wa tani 296.3 ndani ya siku 30
tangu kuachiwa na mahakama.
Mbali na barua hiyo mahakama kuu
imeambatanisha nakala ya umri ya kuuza samaki hao uliotolewa Desemba 11
na jaji Radhia Sheikh hukumu ya kuwaachia huru mahakama ya rufani na
hati ya mkurugenzi wa mashtaka nchini ya kuwafutia mashtaka.
MWANANCHI
Shirikisho la soka Tanzania TFF limepata nguvu kwani linatarajia kupata dola milioni 1.3 sawa na bilioni 2.2 kutoka kwa Shirikisho la soka duniani FIFA pamoja na fedha za kuiandaa timu ya Taifa ya Tanzania kushirikia mshindano ya kombe la dunia mwaka 2018.
Katibu wa FIFA Jerome Valcke alisema
Shirikisho hilo limepanga kuwapa wanachama wake bonasi ya bilioni 2.2
ikiwa ni sehemu ya mapato yake iliyoyapata baada ya kombe la dunia la
Brazil kumalizika mwaka jana.
Mbali na fedha hizo pia FIFA itatoa
milioni 10 kwa kila mwanachama katika kuziandaa timu zao za Taifa kwa
ajili ya kombe la dunia.
MWANANCHI
Baadhi ya wanawake wa Kitanzania
waliofungwa katika magereza ya China na Hong Kong walishika mimba kama
moja ya mbinu za kutumia kupitisha dawa za kulevya bila kugundulika
kwenye uwanja wa ndege na mipaka mingine ya kimataifa.
Watanzania wanne walioko katika Magereza
ya China na Hong Kong walijifungua watoto kwa nyakati tofauti wakiwa
wanatumikia vifungo na wamekiri kuwa walibeba ujauzito kama mbinu ya
kuwasaidia kusafirisha dawa hizo bila kukaguliwa.
Watoto wanaozaliwa magerezani baada ya
kufikisha mwaka mmoja hupelekwa katika vituo vya watoto yatima na
kusomeshwa na Serikali ya China hadi pale wazazi wao watakapomaliza
kutumikia adhabu.
Imebainika kuwa watoto wawili wapo
katika vituo hivyo,mmoja tayari yupo Tanzania baada ya kurudishwa na
bibi yake na mwingine bado yupo gerezani na mama yake.
MWANANCHI
Polisi imewakamata vijana 510 wanaodaiwa kujihusisha na mtandao wa uhalifu maarufu kama Panya Road katika Wilaya za Kinondoni,Ilala na Temeka.
Wazazi na walezi wa watuhumiwa hao
wameonywa kutokwenda kwenye vituo walivyohifadhiwa vijana hao hadi
polisi watakapojiridhisha na upelelezi.
Januari 2 maeneo mbalimbali ya Jiji
yalikumbwa na taharuki kubwa kwa saa 2 baada ya kuwepo na uvumi wa
kuwepo kwa kundi hilo mitaani na kupora mali za watu.
Baada ya tukio hilo Polisi waliendesha msako mkali na kuwakamata vijana 36 wenye rekodi ya kufanya uhalifu.
Jana Kamanda Kova alisema watuhumiwa
wengine 510 walikamatwa katika maeneo mbalimbali ya vijiweni na wengine
wakifuatwa katika nyumba wanazoishi baada ya polisi kupata taarifa za
kiintelijensia.
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.