HOME
Watoto hawa hawakuamini wanachokisikia kuhusu elimu ya uzazi, tazama video hapa
Kulingana na ukuaji wa teknolojia watoto
wadogo wamekuwa na uelewa wa mambo mengi, japo sio vizuri wakajua kila
kitu wakiwa na umri mdogo, je kama mzazi ulishawahi kukaa na mtoto
wako ukajaribu kumdadisi kama anauelewa wa kujua jinsi mtoto
anavyopatikana?
Hiyo ni elimu kubwa kidogo na hata watu wazima kuna mazingira ambayo sio rahisi wakakaa kuyazungumzia, kutoka Marekani team ya cut.com imebuni kipindi cha mazungumzo na watoto, kinaitwa “Birds and the Bees Talk” ambacho wazazi huzungumza ukweli na watoto wao ishu mbalimbali.
Swali ambalo limeulizwa kwa watoto hawa ni kuhusu kupima utashi wao wanaelewa nini kuhusu namna mtoto anavyopatikana?
Baadhi ya watoto walijibu kwamba Mungu
alituma mtoto kwenye tumbo la mama ili waweze kuzaliwa, na wengine
wakajibu wanavyohisi ni sawa, shida ikawa pale walipoelezwa ukweli!
Icheki video na picha zao wakati wa mjadala huo mtu wangu.
Chapisha Maoni