Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars May 29 2016 ilicheza mchezo wake wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Kenya Nairobi Kenya, Taifa Stars ilicheza mchezo huo pasipo kuwepo kwa nyota wake kadhaa akiwemo nahodha wake Mbwana Samatta ambaye leo May 29 2016 alikuwa anamalizia kucheza mechi za PlayOff.
Taifa Stars ikiwa ugenini katika mchezo huo wa kirafiki, ilifanikiwa kufunga goli la uongozi dakika ya 33 kupitia kwa mshambuliaji wake anayeichezea klabu ya Stand United Elias Maguli, ambaye katika Ligi Kuu Tanzania bara amefanikiwa kufunga magoli 14 pia.
Wakati Taifa Stars ambao wanajiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kucheza AFCON dhidi ya timu ya taifa ya Misri watakaocheza June 4 uwanja wa Taifa Dar es Salaam, walilazimishwa sare ya goli 1-1, hiyo inatokana na Kenya kupata goli la penati dakika ya 38 kupitia kwa nahodha wao anayeichezea klabu ya Southampton ya Uingereza Victor Wanyama.
Chapisha Maoni