HOME
Mitihani darasa la saba kuanza leo
Hayo yalisemwa na Kamishna wa Elimu, Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Profesa Eustella Peter jana jijini Dar
es Salaam wakati wa uzinduzi wa wiki ya ukaguzi wa shule za msingi.
Profesa Eustella alisema kati ya wanafunzi hao,
783,223 ni wa shule za kawaida zinazotumia lugha ya Kiswahili katika
kufundishia na 24,888 ni shule zinazotumia Kiingereza na tayari mitihani
imeishapelekwa sehemu husika.
Wanafunzi waliosajili kufanya mtihani huo ni
pungufu ya waliofanya mtihani huo mwaka jana. Waliofanya mtihani huo
walikuwa 844,938.
Alisema kinachosubiriwa kwa sasa ni kufanyika kwa
mitihani hiyo na ufaulu unatarajiwa kuongezeka mwaka huu kutoka asilimia
50.1 ya mwaka jana hadi asilimia 70 mwaka huu, kiwango ambacho ni
sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
Wakati wa ufunguzi wa wiki ya ukaguzi wa shule,
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Shukuru Kawambwa alisema
kuwa, idara hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi, ikiwa ni pamoja na
ripoti za wakaguzi kubaki katika makabati ya wahusika bila mapendekezo
yao kufanyiwa kazi.
“Kuna hili tatizo, wakaguzi wanafanya kazi yao
vizuri, wanatoa mapendekezo ya mambo ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi na
wamiliki wa shule, lakini cha ajabu hakuna lolote linalofanyika,”
alisema.
Chapisha Maoni