HO
Boss alibebwa na wakulima ili viatu visiharibike kwenye barafu, kilichofuatia ni story!
Picha zilizoenea kwenye mitandao ya
kijamii Uturuki zikimuonyesha kiongozi wa Idara ya Huduma Vijijini akiwa
amebebwa juu na wakulima ili kukwepa barafu zilimponza, ikaamriwa
asimamishwe kazi.
Afisa huyo, Nedim Zunarci
alionekana amebebwa na wakulima hao katika Jimbo la Manisa wakati
akikagua athari zilizosababishwa na barafu aliyoanguka kutokana na
baridi kali, akahofia viatu vyake vitaharibika kutokana na barafu hiyo,
hivyo akabebwa na wakulima hao.
Meya wa Manisa, Cengiz Ergun alisema kitendo hicho hakiendani na utaratibu wa kazi wala maadili, pia hakionyeshi uhusiano mzuri kati ya viongozi na jamii.
Comments za watu kwenye mitandao ya kijamii Uturuki walionekana kukosoa pia kitendo hicho baada ya picha hiyo kuzagaa.
ME
Chapisha Maoni