Unknown Unknown Author
Title:
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
HOME VIONGOZI MBALIMBALI WA AFRIKA WAJITOKEZA KUMZIKA MTOTO WA RAILA ODINGA NCHINI KENYA T   Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila ...
HOME

 Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga (wa pili kutoka kulia) akizungumza jambo na ujumbe kutoka Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli. Ujumbe huo ulikwenda kumpa pole nyumbani kwake Bondo nje kidogo ya mji wa Kisumu nchini Kenya kufuatia kifo cha mtoto wake Fidelis Castro Odhiambo Odinga aliyefariki ghafla mapema mwezi huu.
 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akimfariji mama mzazi wa marehemu Fidelis Castro Odhiambo Odinga
 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akizungumza na wafiwa, Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Mheshimiwa Raila Odinga pamoja na Mkewe Mama Ida Odinga
 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akisalimiana na Mke wa Rais wa zamani wa Uganda Mama Miria Obote aliyehudhuria pia katika msiba huo Bondo nchini Kenya.
 Shabiki maarufu wa Timu ya Gor Mahia ya Kenya akilia kwa uchungu katika ibada ya kumuombea marehemu Fidelis Castro Odhiambo Odinga mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga aliyefariki mwanzoni mwa mwaka huu.

Taaswira katika jukwaa kuu.

Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akihutubia maelfu ya Wakenya waliofika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha JOOUST  kwa ajili ya ibada ya Mazishi ya Fidel Odinga.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top