Baada ya kumalizika kwa michezo ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kushuhudia klabu kutoka mji mmoja Real Madrid na Atletico Madrid zikifanikiwa kufika hatua ya fainali ya UEFA 2016, jina la refa atakayechezesha mchezo huo limetangazwa kuwa ni Mark Clattenburg kutoka Uingereza.
Mark Clattenburg mwenye umri wa miaka 41 alitangazwa kuwa refa wa kimataifa toka mwaka 2007, lakini siku saba kabla ya kuchezesha mchezo huo wa fainali katika jiji laMilan Italia, atachezesha mchezo wa fainali ya FA Cup Uingereza May 21 kati ya Man United dhidi ya Crystal Palace katika uwanja wa Wembley.
Clattenburg ni moja kati ya marefa bora kwa sasa lakini aliwahi kufurahisha watu pale alipoingia uwanjani akiwa kasahau kadi, wakati faulo inatokea anaangalia mfukoni anajikuta hana kadi hadi alipoletewa.
UNAWEZA TAZAMA TUKIO LENYEWE MTU WANGU
Chapisha Maoni